• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waokoaji nchini Kenya wapata alama kutoka kwenye ndege iliyopotea

    (GMT+08:00) 2018-06-06 18:53:38

    Waokoaji nchini Kenya wamepata alama kutoka kwenye ndege iliyopotea katika msitu wa Aberdares katikati mwa nchi hiyo.

    Waokoaji kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Kenya, kitengo cha Uchunguzi wa ajali za ndege, polisi na Shirika la Kuhudumia Wanyamapori na wadau wengine wanafanya msako kwenye eneo hilo lililopo mkoa wa kaskazini magharibi wa Kinangop.

    Hata hivyo, hakuna taarifa yoyote kama kuna watu walionusurika kwenye ajali hiyo.

    Taarifa iliyotolewa na kampuni ya East African Safari Air Express imesema, ndege hiyo ilikuwa na abiria wanane na wahudumu wawili, na ilipoteza mawasiliano jana mchana wakati ikitokea Kitale, kaskazini magharibi mwa Kenya kuelekea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako