• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Sekta ya madini yaingiza dola milioni 373

    (GMT+08:00) 2018-06-06 19:44:27

    Mauzo ya madini nchini Rwanda yameongezeka kwa asilimia 124 katika mda wa mwaka mmoja.

    Takwimu kutoka kwa wizara ya madini imeonyesha Rwanda imeingiza dola milioni 373 mwaka 2017 kutoka 166 mwaka uliopita.

    Mapato hayo yameshinda matarajio ya dola milioni 240 kwa mujibu wa wizara ya madini.

    Bei bora za kimataifa za madini zimechangia ongezeko hilo baada ya kupatikana kwa jukwaa bora la biashara.

    Rwanda inalenga kufikisha dola milioni 800 za mauzo ya madini kufikia mwaka 2020.

    Utafiti nchini humo unaonyesha Rwanda itapata madini mengine ya mfumo wa gesi ya methane katika Ziwa Kivu yauayotarajiwa kuongeza mapato.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako