• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Kyrgyzstan wakutana

    (GMT+08:00) 2018-06-06 20:50:34

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na rais Sooronbay Zheenbekov wa Kyrgyzstan, ambapo wamekubaliana kuanzisha uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili, na kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kirafiki.

    Kwenye mazungumzo hayo, rais Xi amesisitiza kuwa kuanzishwa kwa uhusiano huo ni msingi muhimu katika historia ya uhusiano kati ya pande hizo mbili, na kwamba China inapenda kushirikiana na Kyrgyzstan kuhimiza maendeleo ya pamoja, ili kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

    Rais Zheenbekov amesema, Kyrgyzstan itafuata kwa imani thabiti sera ya kuwepo kwa China moja, pia inapenda kuimarisha ushirikiano wenye ufanisi na China katika sekta ya uchumi, biashara na utamaduni, na kulinda kwa pamoja amani, utulivu na usalama kwenye kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako