• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yachukua hatua kudhibiti mauaji ya kisasi dhidi ya wanyamapori

    (GMT+08:00) 2018-06-07 09:39:09

    Tanzania inajitahidi kuzuia mauaji ya wanyamapori ya kulipiza kisasi katika maeneo ya hifadhi baada ya simba tisa kuripotiwa kuuawa katika kijiji cha Nyichoka, karibu na mbuga ya kitaifa ya Serengeti.

    Katibu Mkuu wa Wizara ya maliasili na utalii Bw Bw. Gaudence Milanzi amesema licha ya kuzindua kikosi cha kupambana na ujangili, serikali pia itaanza kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi wanyamapori na mazingira.

    Pia amesema mauaji kama hayo yanayotokana na migongano kati ya binadamu na wanyamapori yameongezeka, na hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa ili kuzuia hali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako