• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya misaada yataka kupata nafasi ya kuwafikia wenye mahitaji Sudan Kusini ili kuepusha njaa

    (GMT+08:00) 2018-06-07 09:48:58

    Mashirika ya misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini yametoa mwito kwa pande zinazopambana nchini humo kuacha uhasama na kutoa nafasi zaidi ya kuwafikia watu wanaohitaji msaada katika kipindi chenye mavuno kidogo.

    Katibu mkuu wa baraza la wakimbizi la Norway Bw Jan Egeland amewaambia waandishi wa habari mjini Juba kuwa raslimali zaidi zinahitajika na msaada zaidi unahitajika ili kuepuka janga la njaa nchini Sudan Kusini.

    Mfumo wa kutabiri njaa wa nchi hiyo umetabiri kuwa watu milioni 7.1 wa Sudan Kusini wanakabiliwa na njaa, kutokana na kuwa watu milioni 4.5 wamekimbia makazi yao tangu mwaka 2013. Amesema licha ya Sudan kuwa na uwezo wa kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula wakulima wengi wamekimbia ili kutafuta usalama kwenye kambi za wakimbizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako