• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN-ECA: Ukuaji mkubwa wa uchumi Afrika wachangia kidogo katika kupunguza umaskini

    (GMT+08:00) 2018-06-07 10:37:41

    Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika UN-ECA imesema ukuaji mkubwa wa uchumi ulioshuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni kwenye nchi nyingi za Afrika, umetoa mchango mdogo katika kupunguza umaskini.

    Akizungumza kwenye mkutano wa wataalamu wa tume ya ECA kuhusu "umaskini, ukosefu wa usawa na ajira barani Afrika" uliofanyika jana mjini Addis Ababa, mkuu wa kitengo cha ajira na huduma za kijamii cha tume hiyo Saurabh Sinha amesema umaskini barani Afrika unapungua kwa kasi ndogo zaidi kuliko sehemu nyingine duniani tangu mwaka 1990. Amesema umaskini ulipungua kutoka asilimia 54.3 ya mwaka 1990 hadi asilimia 41 ya mwaka 2013, na idadi ya watu wanaoishi katika umaskini mkubwa iko sawa na ile ya mwaka 2002.

    Kwa mujibu wa ECA, umaskini, ukosefu wa usawa na ukosefu wa ajira bado ni changamoto kubwa barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako