• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasema ndege iliyopotea imeonekana msituni

    (GMT+08:00) 2018-06-07 18:47:56

    Mabaki ya ndege ndogo iliyopotea katika msitu wa Aberdares katikati ya Kenya jumanne wiki hii yamepatikana mapema leo.

    Katibu wa Kudumu wa Wizara ya Uchukuzi nchini Kenya Paul Maringa amesema, ndege hiyo imegunduliwa na timu ya waokoaji kwa kutumia ndege.

    Ndege hiyo, Fly-SAX, iliyokuwa na abiria 10, wakiwemo wahudumu wawili, ilikuwa ikitokea uwanja wa ndege wa Kitale magharibi mwa Kenya kuelekea mjini Nairobi ilipopoteza mawasiliano na chumba cha uongozaji wa ndege.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako