• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasema China imekuwa nchi kubwa ya pili ya uingizaji wa fedha za kigeni

    (GMT+08:00) 2018-06-07 21:01:36

    Mkutano wa Biashara na Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCTAD) umesema, China imekuwa nchi kubwa ya pili kwa kuingiza fedha za kigeni, na nchi kubwa ya tatu ya uwekezaji wa kigeni duniani katika mwaka 2017, na inaendelea kuwa nchi kubwa kwa nchi zinazoendelea katika sekta hizo.

    Hayo yamo kwenye ripoti ya uwekezaji duniani ya mwaka 2018 iliyotolewa katika mkutano huo, na kuongeza kuwa tofauti na ukuaji haraka wa uchumi na biashara ya dunia ya mwaka 2017, uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) ulipungua hadi asilimia 23 kutoka mwaka 2016 ambao umefikia dola za kimarekani milioni 1.43.

    Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji ya UNCTAD Bw. Zhan Xiaoning amesema, hivi karibuni China imetangaza mfululizo wa hatua za kurahisisha na kukuza uwekezaji, na uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni nchini China unatarajiwa kuendelea katika kiwango cha juu katika siku za mbele.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako