• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia haina mpango wa kuondoa vikosi vyake kutoka Syria katika siku za karibuni

    (GMT+08:00) 2018-06-08 09:53:49

    Rais Vladmir Puti wa Russia amesema nchi yake haina mpango wa kuondoa vikosi vyake kutoka Syria katika siku za hivi karibuni, lakini hali ikiruhusu inaweza kuondoa vikosi vyake mara moja.

    Akiongea kwenye kipindi cha televisheni cha moja kwa moja cha maswali na majibu, Rais Putin amesema jeshi la Russia litaendelea kuwepo Syria kama kuna manufaa kwa Russia na kutekeleza wajibu wake kimataifa. Amesema ushiriki wa Russia katika mapambano dhidi ya ugaidi ni jambo muhimu na la fahari kwa Russia, lenye lengo la kulinda maslahi ya Russia na wananchi wake. Amesema kuna magaidi wengi kutoka Russia na sehemu nyingine za Asia ya kati waliosongamana nchini Syria.

    Kwa sasa Russia ina vituo viwili vya kijeshi vilivyowekwa kwa idhini ya serikali ya Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako