• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Trump asema anapenda kumwalika Kim Jong Un kufanya ziara nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2018-06-08 09:54:46

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema anapenda kumwalika kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kufanya ziara nchini Marekani, kama mazungumzo kati yao nchini Singapore yatafanyika vizuri.

    Rais Trump aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kukutana na waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe. Rais Trump amesema anatumai kuwa uhusiano kati ya Marekani na Korea Kaskazini utarudi kwenye njia ya kawaida, na masuala yote yanayofuatiliwa na pande mbili yatatatuliwa.

    Habari nyingine zinasema, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo amesema baada ya mazungumzo kati ya wakuu wa Marekani na Korea Kaskazini tarehe 12 Juni, atafanya ziara nchini Korea Kusini na China kuziarifu nchi hizo kuhusu hali ya mazungumzo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako