• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi wanachama wa SCO kuimarisha ushirikiano dhidi ya changamoto za usalama

  (GMT+08:00) 2018-06-08 17:08:02

  Nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO wataimarisha ushirikiano ili kukabiliana na changamoto za ugaidi, dawa za kulevya na uhalifu wa kuvuka mipaka na matishio ya usalama wa habari.

  Mkurugenzi wa idara ya ushirikiano wa kimataifa ya wizara ya usalama wa umma ya China Bw. Liao Jinrong amesema hayo alipokutana na waandishi wa habari kabla ya mkutano wa kilele wa 18 wa Jumuiya ya SCO utakaofanyika mjini Qingdao wikiendi hiii, huku akiongeza kuwa jumuiya hiyo inatunga hatua za kutatua changamoto hizo.

  Bw. Liao pia amesema, ugaidi ni changamoto kubwa zaidi ya usalama inayolikabili SCO, na katika miaka kadhaa iliyopita, nchi wanachama wa jumuiya hiyo zimepata maendeleo katika kuzuia mashambulizi ya kigaidi na kukamata magaidi wanaotoka kwenye makundi ya kigaidi ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako