• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Li Zhanshu akutana na Rais wa Kazakhstan

  (GMT+08:00) 2018-06-08 17:10:14

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China Bw. Li Zhanshu amekutana na Rais Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan hapa Beijing.

  Katika mazungumzo yao, Bw. Li amesema mashirika ya kisheria ya nchi hizo mbili yanapaswa kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo, kudumisha na kuimarisha mawasiliano ya kiuchumi na kisiasa ili kutimiza malengo yao ya kimkakati ya kitaifa, na kuhimiza uhusiano wa nchi hizo mbili kuendeleza katika kiwango cha juu zaidi.

  Rais Nazarbayev amesema, nchi yake ina nia ya kuimarisha ushirikiano wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kuunga mkono ushirikiano kati ya mashirika ya kisheria ya nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako