• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU yazindua ripoti kuhusu maendeleo ya teknolojia kwa ajili ya maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2018-06-09 19:18:26

    Idara kuu ya Umoja wa Afrika inayoshughulikia maendeleo ya uvumbuzi wa kiteknolojia APET, jana imezindua ripoti kuhusu kuibuka kwa uvumbuzi mwingi ambao unaaminika kuwa umesaidia katika maendeleo endelevu kiuchumi na kijamii, pamoja na mageuzi ya kimfumo barani Afrika.

    Kwa kushirikiana na washirika wapya wa maendeleo barani Afrika NEPAD pamoja na Tume ya Umoja wa Afrika, APET huishauri AU kuhusu maendeleo ya vumbuzi za kiteknolojia ili kuiwezesha sekta ya sayansi barani Afrika kuwa ya kiushindani na ichangie kufanikisha malengo ya mkakati wa maendeleo ya Afrika kupitia sayansi, teknolojia na Uvumbuzi (STISA) 2014-2024.

    Ripoti zilizozinduliwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa uvumbuzi mjini Kigali nchini Rwanda kuanzia Juni 6 hadi juni 8, ziliangazia zaidi mapambano dhidi ya malaria pamoja na namna ya kuuondoa ugonjwa huo, jinsi ya kuongeza uzalishaji kupitia kilimo na kuinua upatikanaji wa nishati barani Afrika.

    Taarifa zinasema kwamba, ripoti hizo zilizotolewa ni rasilimali zenye thamani katika kuendeleza uvumbuzi wa kiteknolojia na kujenga utamaduni wa kisayansi, teknolojia na uvumbuzi barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako