• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa 18 wa kamati ya viongozi wa SCO wafanyika mjini Qingdao, China

  (GMT+08:00) 2018-06-10 17:22:47

  Mkutano wa 18 wa kamati ya viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai SCO umefanyika leo mjini Qingdao, China. Baada ya kumaliza ajenda zote, viongozi waliohudhuria mkutano huo walikutana na waandishi wa habari, huku rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba ya kujulisha matokeo ya mkutano huo.

  Rais Xi amesema kwenye mkutano huo pande mbalimbali zimeamua kufuata kwa makini kanuni ya Katiba ya SCO, kueneza moyo wa Shanghai wa usawa, kuaminiana, kunufaishana, kushauriana, kuheshimiana, na kutafuta maendeleo ya pamoja. Anasema, "Viongozi wa nchi wanachama na waangalizi wa SCO na wakuu wa mashirika husika ya kimataifa wamekutana mjini Qingdao, wamepanga kwa pamoja mpango wa maendeleo ya SCO katika zama mpya, na kubadilishana maoni kuhusu masuala muhimu ya kikanda na kimataifa, na kufikia makubaliano mengi."

  Kwenye mkutano huo, viongozi wa SCO wamesaini nyaraka mbalimbali zikiwemo Taarifa ya Qingdao ya Kamati ya Viongozi wa SCO, Taarifa ya Pamoja ya Viongozi wa SCO kuhusu Kurahisisha Biashara, na muongozo kwa ajili ya utekelezaji wa Makubaliano ya Ushirikiano wa Ujirani Mwema wa Muda Mrefu wa Nchi Wanachama wa SCO katika miaka mitano ijayo. Rais Xi anasema, "Tumekubaliana kuwa usalama ni msingi wa maendeleo endelevu ya SCO. Pande mbalimbali zitafuata nyaraka za ushirikiano zikiwemo makubaliano ya Shanghai dhidi ya ugaidi, ufarakanishaji na msimamo mkali, ili kulinda usalama na utulivu wa kikanda."

  Rais Xi amesema pande zote za SCO zimekubali kuwa utandawazi ni mwelekeo usiobadilika, zitalinda utaratibu wa Shirika la Biashara Duniani, na kupinga kithabiti kitendo chochote cha kujilinda kibiashara. Aidha, nchi wananchama wa SCO zitaongeza mawasiliano na ushirikiano na pande nyingine za kimataifa. Anasema,"Historia na ustaarabu wa nchi mbalimbali ni mali za binadamu wote. Pande mbalimbali za SCO zinapenda kuongeza ushirikiano wa pande mbili na pande nyingi katika utamaduni, elimu, sayansi, uhifadhi wa mazingira, afya, utalii, vijana, vyombo vya habari, michezo na nyinginezo. Aidha, SCO pia itaongeza mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa, ili kuhimiza amani ya kudumu na ustawi wa pamoja duniani."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako