• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa Ethiopia asema Ethiopia haitaathiri mgao wa maji ya mto Nile kwa Misri

    (GMT+08:00) 2018-06-11 09:11:53

    Waziri Mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed Ali, amesema Ethiopia haitaathiri mgao wa maji ya mto Nile kwa Misri kutokana na ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme la GERD.

    Akiongea mjini Cairo kwenye mkutano wa pamoja na Rais Abdel Fatah al-Sisi wa Misri baada ya kufanya mazungumzo, Waziri mkuu huyo amemhakikishia Rais al-Sisi kuwa Ethiopia haitaleta madhara yoyote kwenye mgao wa maji ya mto huo kwa Misri kutokana na ujenzi wa bwawa la umeme.

    Kumekuwa na wasiwasi kuwa ujenzi wa bwawa la GERD nchini Ethiopia ambao utakuwa na manufaa makubwa ya kiuchumi kwa Ethiopia, utapunguza mgao wa maji kwa mita bilioni 55.5 za ujazo kwa Misri.

    Rais al-Sisi amesema uhusiano kati ya Misri na Ethiopia ni wa kimkakati, na kuahidi kuwa Misri itaendelea na ushirikiano na Ethiopia kwa manufaa ya nchi mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako