• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na Iran kuimarisha ushirikiano

  (GMT+08:00) 2018-06-11 09:25:41

  Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Iran Bw. Hassan Rouhani wamefanya mazungumzo na kukubaliana kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zao.

  Marais hao wawili wamefikia makubaliano hayo kwenye mazungumzo waliyofanya baada ya kuhudhuria mkutano wa 18 wa kilele wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai SCO mjini Qingdao, mashariki mwa China.

  Rais Xi Jinping amezitaka China na Iran ziimarishe ushirikiano kwenye "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuhimiza ushirikiano wa utekelezaji sheria na usalama kutokana na mapambano dhidi ya ugaidi, kuzidisha mawasiliano na ushirikiano kati ya wananchi wao, na kuhimiza urafiki kati ya nchi hizo mbili.

  Rais Rouhani amesema makubaliano ya nyuklia ya Iran hivi sasa yanakabiliwa na changamoto, na Iran inaitaka jumuiya ya kimataifa ikiwemo China itoe michango ya kiujenzi katika kushughulikia masuala husika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako