• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Putin autaja ushirikiano kati ya Russia na China kuwa muhimu kwa mahusiano ya kimataifa

  (GMT+08:00) 2018-06-11 09:31:35

  Rais Vladimir Putin wa Russia amesema uratibu kati ya Russia na China uko kwenye kiwango cha juu, na unatakiwa kuendelezwa, kitu ambacho sio tu kitanufaisha uhusiano wa pande hizo mbili, bali pia kina umuhimu mkubwa kwa mahusiano ya kimataifa katika zama hizi.

  Rais Putin amesema hayo akizungumza na wanahabari kuhusu matunda ya ziara yake nchini China na mustakbali wa maendeleo ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO. Amesema Russia na China zimefanya uratibu wa kina katika majukwaa ya Umoja wa mataifa, kundi la G20, kundi la nchi za BRICS, na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai. Pia amerudia msimamo wake wa kuunganisha Umoja wa Kiuchumi wa Ulaya na Asia na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na anaona kufanya hivyo ni hatua muhimu ya kuzidisha uhusiano kati ya Russia na China.

  Akizungumzia matokeo ya mkutano wa kilele wa SCO uliomalizika huko Qingdao na mustakbali wa maendeleo yake, rais Putin amesema mkutano huo umegusia masuala ya mapambano dhidi ya ugaidi na usalama, na kufuatwa kanuni za biashara za kimataifa. Amesema kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa, uwezo wa manunuzi wa SCO sasa umeupiku ule wa kundi la G7.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako