• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi Tanzania wazindua msako dhidi ya wauaji wa wanyamapori

    (GMT+08:00) 2018-06-11 09:45:30

    Polisi nchini Tanzania wanamsaka mtu aliyedaiwa kuwaua pundamilia wawili kwenye barabara kuu ya Arusha-Nairobi.

    Ofisa wa wanyamapori wa Wilaya ya Longido Bw. Peter Kubingwa, amesema tukio hilo lilitokea Jumamosi asubuhi kwenye eneo la Namanga, karibu na mpaka kati ya Tanzania na Kenya.

    Bw. Kubingwa alisema mwendesha gari ametambuliwa kuwa ni Deogratius Beatus Loya ambaye ni mkazi wa Arusha. Bw. Kubingwa amelaumu dereva huyo kwa kukimbia na kuacha gari lake baada ya tukio hilo. Pia ametoa wito kwa madereva wanaotumia barabara kuu kuwa macho wanapopita kwenye ushoroba wa vivuko vya wanyamapori, na kuwa makini kwa kufuata alama za barabarani.

    Kati ya mwaka 2011 na 2015, wanaymapori 956 wa hifadhi ya taifa ya Mikumi walikufa kutokana na ajali ya barabarani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako