• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini utalenga kuanzisha mfumo wa kudumu wa amani

  (GMT+08:00) 2018-06-11 20:42:23

  Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA) limesema, mazungumzo kati ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un na rais Donald Trump wa Marekani yatalenga kuanzisha mfumo wa kudumu wa amani na suala la kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye Peninsula ya Korea.

  Shirika hilo limesema, viongozi hao watabadilishana maoni katika masuala ya kuanzisha uhusiano mpya kati ya Korea Kaskazini na Marekani, na masuala mengine yanayofuatiliwa kwa pamoja na pande hizo mbili, kama inavyotakiwa na zama hizi zilizobadilika.

  Viongozi hao waliwasili nchini Singapore jana kwa ajili ya mkutano wao unaotarajiwa kufanyika kesho katika kisiwa cha Sentosa.

  Huu utakuwa mkutano wa kwanza kati ya rais wa Marekani aliye madarakani na kiongozi wa Korea Kaskazini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako