• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tetesi za Usajili wa Wachezaji: Lakers wadaiwa kujipanga kwa ajili ya kumnunua Lebron James

  (GMT+08:00) 2018-06-12 09:19:50

  Baada ya ligi ya kikapu nchini Marekani kumalizika na baada ya timu yake kufungwa kwenye mechi za fainali kuu, mchezaji Lebron James wa Cleveland Cavaliers sasa ndiyo anatazamwa zaidi kuhusu hatma yake wakati huu ambapo anamaliza mkataba na timu yake.

  Wakati watu wakijiuliza kwamba atabaki katika timu yake hiyo au atakwenda wapi, tayari kuna tetesi kuwa dau nono lililoandaliwa na Los Angeles Lakers huenda likamvuta kujiunga nayo hasa wakati huu ambapo timu hiyo imetangaza kujipanga kwa ajili ya ubingwa msimu ujao.

  James ambaye ni mzaliwa wa Ohio alijiunga kwa mara ya kwanza na timu ya Clevelend mwaka 2003 akiitumikia kwa miaka 7 hadi mwaka 2010 alipohamia Miami Heat na baadaye akirejea tena Clevelend mwaka 2014 na kuipa ubingwa mwaka 2016 ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka 46.

  Lakini kila akiulizwa hatma yake, James anasema bado anatafakari sasa kutokana na sababu mbalimbali, hasa za kifamilia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako