• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AMISOM yaimarisha operesheni nchini Somalia baada ya kituo cha jeshi kushambuliwa

  (GMT+08:00) 2018-06-12 09:48:50

  Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imesema,iumeimarisha operesheni za usalama mjini Mogadishu na katika sehemu za karibu ili kuwafurusha wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab wakati mwezi wa Ramadhani ukimalizika wiki hii.

  Tume hiyo imesema operesheni za usalama zitafanyika katika sehemu mbalimbali ikiwemo Hawahabid, Lafoole, Afgoye, Albao na Lantabur kusini mwa Mogadishu, ili kupambana na wapiganaji wanaoshambulia vikosi vya Somalia na washirika wake karibu kila siku.

  Operesheni hizo zinafanyika baada ya kundi hilo lenye itikadi kali kufanya shambulizi dhidi ya kituo cha jeshi la Somalia huko Siinka Dheer pembezoni mwa Mogadishu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako