• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shughuli za hakimiliki za ujuzi nchini China zaendelea kwa utulivu

  (GMT+08:00) 2018-06-12 16:58:28

  Kituo cha utafiti wa maendeleo ya shughuli za hakimiliki za ujuzi cha China, leo kimetoa ripoti ikisema mwaka jana China ilipata maendeleo yenye utulivu katika shughuli za hakimiliki za ujuzi, na kusonga mbele duniani.

  Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa maendeleo ya shughuli za hakimiliki za ujuzi cha idara ya hakimiliki ya ujuzi ya China Bw. Han Xiucheng, amesema ripoti iliyotolewa leo na kituo hicho imetathmini na kuchambua hali ya maendeleo ya shughuli za hakimiliki ya ujuzi katika sehemu nne za uvumbuzi, matumizi, uhifadhi na mazingira, na kuhitimisha kuwa mwaka jana shughuli za hakimiliki za ujuzi nchini China zilipata maendeleo dhahiri. Bw. Han anasema,

  "Takwimu zinaonesha kuwa mwaka jana kasi ya kuinuka kwa kiwango cha uvumbuzi nchini China iliongezeka, na faharisi ya kiwango hicho imeongezeka na kuwa 216.5 kutoka 189.5 ya mwaka 2016. Mwaka jana idadi ya maombi na uandikishaji wa hakimiliki za ujuzi za aina mbalimbali iliongezeka kwa kiasi kikubwa, na muundo pia uliboreshwa."

  Ripoti hiyo imesema, mwaka jana idadi ya maombi ya hataza ilifikia milioni 1.382, ambalo ni ongezeko la asilimia 14.2 ikilinganishwa na mwaka 2016, na kushika nafasi ya kwanza duniani kwa miaka 7 mfululizo. Wakati huo huo mwaka jana China pia ilishughulikia maombi milioni 574.8 ya chapa za kibiashara, ambalo ni ongezeko la asilimia 55.72 kuliko mwaka 2016, na idadi hii pia ni ya kwanza duniani kwa miaka 16 mfululizo. Bw. Han anasema,

  "Marekani na Japan zinashika nafasi za mbele zaidi duniani katika kiwango cha maendeleo ya shughuli za hakimiliki za ujuzi, China inashika nafasi ya katikati na mbele duniani. Mwaka 2016 China ilisonga nafasi yake mbele kuwa 10 kutoka 14 kwa kuzihinda Denmark, New Zealand na nchi nyingine mbili. Shughuli za hakimiliki za ujuzi nchini China zinaendelea kwa kasi, haswa juhudi za kuhifadhi na kutumia hakimiliki za ujuzi zimepiga hatua kubwa. Hata hivyo mazingira ya hakimiliki za ujuzi nchini China bado yako nyuma ikilinganishwa na nchi zilizoendelea zaidi."

  Aidha, ripoti hiyo imesema hivi sasa China bado inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na uwiano mzuri kati ya mikoa katika kiwango cha maendeleo ya shughuli za hakimiliki za ujuzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako