• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afrika: Wawekezaji wa kigeni wanaogopa kuwekeza kwenye nchi zinazoendelea.

  (GMT+08:00) 2018-06-12 18:25:13
  Wawekezaji wa kigeni wana hofu ya kuwekeza katika nchi hususan zilizoendelea na hivyo kuweka mashakani mafanikio ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

  Katibu Mkuu wa kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi amesema hayo jijini New York, Marekani kwenye mkutano ulioangazia uchangishaji wa fedha kwa ajili ya maendeleo, akitaja miongoni mwa sababu za kusitasita kwa wawekezaji hao.

  Ametaja sababu hizo kuwa ni pamoja na nchi zinazoendelea kupenda miradi ya maendeleo lakini maandalizi yake hayafikii kiwango cha kushawishi wawekezaji kupeleka fedha zao.

  Sababu nyingine ni hali ya kisiasa ambayo Dkt. Kituyi amelinganisha na dhoruba ya kibiashara ambayo inasababisha hofu, shaka na shuku kwa wawekezaji na pia kule ambako miradi inapelekwa. Dkt. Kituyi ametaja pia baadhi ya viongozi wa kisiasa bado hawajaona uhusiano wa vitegauchumi vya kigeni nchini mwao, FDIs na malengo ya maendeleo endelevu SDGS.

  Kutokana na hili, Kituyi amesema wameandaa kikao maalum kitakachowaleta pamoja viongozi wakuu wa Afrika, mwezi Septemba mwaka huu jijini New York, ambapo viongozi watakaohudhuria watapata fursa ya kuhamasishwa kuhusu uhusiano huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako