• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Viongozi waomba pesa za maendeleo  zisiathiri utekelezaji wa bajeti.

    (GMT+08:00) 2018-06-12 18:25:33
    Wakati Serikali ikitarajia kuanza kutekeleza bajeti mpya, kumbukumbu zinaonyesha baadhi ya wizara hazikupata hata senti moja ya fedha za miradi ya maendeleo mwaka huu wa fedha.

    Utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2017/18 unakamilika Juni 30 na ukusanyaji wa mapato na matumizi kwa mwaka mpya wa fedha utaanza kutekelezwa Julai Mosi.

    Wakati maandalizi hayo yakiendelea kufanyiwa kazi, imebainika kuwa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi pamoja na idara ya mawasiliano iliyo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano hazikupokea fedha zozote kutoka Hazina licha ya kuidhinishwa na bunge mwaka jana. Wakati wizara hizo zikikosa fedha za kufanikisha mipango ya maendeleo, nyingine nyingi zilipewa chini ya nusu ya kiasi kilichoidhinishwa.

    Alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema kati ya Sh31.7 trilioni zilizoidhinishwa, Sh19.7 trilioni zilikuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh11.9 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

    Kutotolewa kabisa kwa fedha za maendeleo kwa baadhi ya wizara huku nyingine zikipata chini ya matarajio ni suala ambalo limepigiwa kelele na wabunge, wachambuzi wa uchumi na wadau wa maendeleo kwamba linakwaza ufanikishaji wa mipango iliyowekwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako