• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yataka mkutano wa viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani kuhimiza kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea

  (GMT+08:00) 2018-06-12 19:19:41

  Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Wang Yi amesema China inawataka viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani waondoeusumbufu, kujenga maelewano, kutatua matatizo na kufikia makubaliano kuhusu kuhimiza na kutimiza hali ya kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea.

  Akizungumza hapa Beijing, Bw. Wang Yi amesema viongozi hao wanapaswa kujenga utaratibu wa amani wa peninsula ya Korea, na kupata mafanikio halisi, na kusisitiza China itaendelea kutoa umuhimu wa kimkakati. Amesema nchi hizo mbili zimepingana kwa zaidi ya nusu karne, hivyo mazungumzo ya usawa kati ya viongozi hao wawili yana umuhimu mkubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako