• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mwenzake wa Ghana

  (GMT+08:00) 2018-06-12 20:18:41

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana amekutana na mwenzake wa Ghana Bibi Shirley Ayorkor Botchway ambaye yuko ziarani hapa China.

  Bw. Wang amesema, China inapenda kushirikiana na Ghana kutumia vizuri jukwaa la mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika mwezi Septemba mwaka huu kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kushauriana, kusaidiana na kushirikiana ili kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

  Bibi Botchway amesema, serikali ya Ghana inazingatia maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hiyo na China na itaendelea kutekeleza sera ya China Moja. Amesema Ghana inapenda kujifunza uzoefu wa maendeleo ya China na kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ili kusukuma mbele ushirikiano wa pande mbili upate maendeleo mapya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako