• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi wa China atembelea kituo cha afya kwa ajili ya watoto wa Somalia

  (GMT+08:00) 2018-06-13 09:36:43

  Balozi wa China nchini Somalia Bw. Qin Jian ametembelea kituo cha afya kilichojengwa na China katika eneo la Wadjiri mjini Mogadishu, ambako watoto elfu 15 wa Somalia wanapata huduma za matibabu.

  Kituo hicho kinaendesha mradi wa matunzo ya mama kwa mtoto na kinaendeshwa na Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa UNICEF, kwa ufadhili wa dola za kimarekani milioni mbili kutoka China.

  Balozi Qin amesema China itaendelea kuisaidia Somalia, na kukumbusha kuwa mbali na msaada huo, pia ilitoa dola milioni 1.5 kuwasaidia watu waliokumbwa na mafuriko, na imetoa misaada ya maendeleo, kibinadamu, amani na udhamini wa masomo.

  Naibu mwakilishi wa UNICEF nchini Somalia Bw. Jesper Moller ameishukuru serikali ya China kwa mchango wake katika ujenzi wa kituo hicho, na kusema msaada wa China umewasaidia watoto 1,500 waliokuwa wanasumbuliwa na utapia mlo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako