• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania-Kiwanda cha Jielong Holdings kuzalisha mafuta kwa wingi

  (GMT+08:00) 2018-06-13 16:03:39
  Kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Shinyanga kinachomilikiwa na Jielong Holdings (T) Ltd,kimejipanga kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo baada ya kusimamisha uzalishaji kwa miezi minne.

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Jerry Qi, aliyasema hayo jana wakati akielezea mikakati ya kiwanda hicho ambacho kilianza kufanya kazi nchini Tanzania mwaka 2013.

  Alisema kuwa awali walisimamisha uzalishaji kwa sababu walipungukiwa na malighafi lakini sasa wana pamba na mbegu za alizeti za kutosha na wameanza kufanya kazi hivi karibuni.

  Aliongeza kuwa tangu kuanza kwa uzalishaji wamekuwa wakisaidia jamii inayowazunguka kama vile kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari na kutoa zana za kilimo kwa wakulima wa wilaya ya Kishapu.

  Qi aliongeza kuwa mafuta yanayozalishwa katika kiwanda hicho yamekuwa yakiuzwa nchini, Kenya na China na kwamba wamejipanga kuzalisha kiwango kikubwa cha mafuta kwa kutosheleza mahitaji ya wananchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako