• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani kufanya ziara China

  (GMT+08:00) 2018-06-13 20:24:08

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang ametangaza kuwa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo atafanya ziara nchini China hapo kesho.

  Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Marekani watabadilishana maoni kuhusu maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani na masuala mengine yanayofuatilia kwa pamoja ya kimataifa na ya kikanda.

  Bw. Geng pia amesema, China na Marekani zikiwa nchi kubwa zaidi kiuchumi, zinapaswa kudumisha maendeleo mazuri ya uhusiano kati yao ili kupata maslahi ya pamoja na kutimiza matarajio ya jumuiya ya kimataifa.

  Hii ni mara ya kwanza kwa Bw. Pompeo kutembelea China tangu kushika wadhifa wake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako