• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la dunia mwaka 2026 kuchezwa Marekani, Canada na Mexico

  (GMT+08:00) 2018-06-14 09:26:51

  Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2026 zitarudi tena barani Amerika Kaskazini baada ya Mkutano Mkuu wa Fifa kuzipa Marekani, Canada na Mexico haki ya kuandaa michuano hiyo mikubwa ya soka duniani. Morocco, ambayo iliingia tena kwenye kinyang'anyiro cha kuwania uenyeji wa fainali hizo baada ya kushindwa mara mbili, ilizidiwa nguvu na umoja huo.

  Michuano hiyo itarudi Amerika Kaskazini miaka 32 baada ya Marekani kuwa mwenyeji wa fainali hizo mwaka 1994. Katika kura zilizopigwa jana Marekani, Canada na Mexico, ambazo zitakuwa nchi tatu za kwanza kuandaa fainali hizo kwa pamoja, zilipata kura 134 (sawa na asilimia 67, wakati Morocco ilipata kura 65 sawa na asilimia 33 ya kura zote. Awali, Morocco iliahidi kuwa iwapo ingepata uenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2026, ingeipa FIFA kiasi cha Dola 5 billioni (sawa na Sh10 trilioni) kama faida itakayopatikana kwenye mashindano hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako