• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wasiopungua kumi wauawa kwenye shambulizi lililotokea kaskazini mwa Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-06-14 10:29:45

    Polisi ya Nigeria imesema watu wasiopungua kumi wamethibitishwa kuuawa katika shambulizi lililofanywa na majambazi kaskazini magharibi mwa Nigeria.

    Habari zinasema watu wengine wengi wamejeruhiwa wakati majambazi hao waliposhambulia vijiji viwili vilivyoko jimbo la Zamfara, kaskazini mwa Nigeria.

    Msemaji wa polisi ya Zamfara Bw Muhammadu Shehu amesema wanausalama wamechukua hatua mara moja baada ya wananchi walioko katika eneo la Birnin-Magaji la jimbo la Zamfara waliposhambuliwa na majambazi. Ameongeza kuwa majambazi hao walikimbilia katika msitu wa Rugu kwenye mpaka kati ya jimbo la Zamfara na Katsina, kaskazini magharibi mwa Nigeria, ambako wamezingirwa na polisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako