• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda yazindua mfuko wa utafiti na uvumbuzi

    (GMT+08:00) 2018-06-14 18:50:06

    Rwanda imezindua mfuko wa utafiti na uvumbuzi.

    Mfuko huo wa Utafiti (NRIF) ulizinduliwa rasmi Jumatano na utafadhiliwa na serikali na utazingatia hasa vijana.

    Uzinduzi uliongozwa na Waziri Mkuu Dr Edouard Ngirente ukihudhuriwa na vongozi wa juu wa serikali, wasomi na watafiti

    Ngirente alifafanua kuwa serikali itagawa sehemu ya bajeti ya kitaifa kwa mfuko huo lakini hakutaa ni kiasi gani cha fedha.

    Mfuko huo utasimamiwa na Baraza la Taifa la Sayansi na Teknolojia lengo kuu likiwa ni kuunganisha sayansi, teknolojia, uvumbuzi na utafiti katika mikakati na mipango ya maendeleo ya kitaifa.

    Rwanda sasa ni kati ya nchi chache za Afrika ambazo zina mfuko sawa na huo baada ya Afrika Kusini, Kenya na Misri.

    Waziri wa Elimu, Eugene Mutimura, alisema kuwa Mfuko huo utawasaidia katika kuimarisha uwezo wenye vipaji na ujuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako