• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Satilaiti ya kupokea na kurusha habari ya Chang'e -4 yaingia mzunguko wa anga ya juu

    (GMT+08:00) 2018-06-14 18:52:27

    Satilaiti ya kupokea na kurusha habari kwa ajili ya chombo cha anga za juu cha Chang'e-4, kinachotarajiwa kutua Mwezini mwishoni mwa mwaka huu, kimeingia kwenye mzunguko wa anga za juu.

    Kituo cha Kusimamia Anga za Juu cha China kimesema, satilaiti hiyo, iitwayo Magpie Bridge, ilirushwa Mei 21 mwaka huu na kuingia kwenye mzunguko wa anga ya juu leo mchana baada ya safari ya zaidi ya siku 20. Rais wa Chuo cha Teknolojia ya Anga za Juu cha China Zhang Hongtai amesema, satilaiti hiyo ni ya kwanza duniani kufanya kazi katika anga ya juu, na itaweka msingi wa Chang'e-4, ambayo inatarajiwa kuwa ya kwanza kutua kwa utulivu Mwezini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako