• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja ni muhimu kwa kuhimiza pande mbalimbali na utandawazi wa dunia wa uchumi

    (GMT+08:00) 2018-06-14 18:57:30
    Kongamano la ngazi ya juu kuhusu pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja na ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 limefanyika jijini New York, Marekani.

    Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na ujumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa, na idara mbalimbali za umoja huo. Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ma Zhaoxu alihudhuria kongamano hilo na kusema, pendekezo hilo linaendana na ajenda ya mwaka 2030 katika kuhimizana na kusukuma mbele ushirikiano wa maendeleo ya kimataifa.

    Balozi Ma amesema, jamii ya kimataifa na nchi na mashirikia ya kimataifa zaidi 100 yanaunga mkono pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja lilitolewa na China. Amesema China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali kutekeleza mafanikio ya baraza la viongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Ukanda Mmoja na Njia Moja na kuwanufaisha zaidi watu wa nchi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako