• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono suala la nyuklia la peninsula ya Korea kuingia njia sahihi ya mazungumzo na ya amani

    (GMT+08:00) 2018-06-14 19:22:19

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi leo hapa Beijing amesema mkutano kati ya rais Donald Trump wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un una umuhimu mkubwa wa kihistoria.

    Amesema mkutano huo umelifanya suala la nyuklia la peninsula ya Korea liingie kwenye njia sahihi ya mazungumzo na ya amani, ambao unaendana na maslahi ya pamoja ya pande mbalimbali zikiwemo Marekani na Korea Kaskazini. Ameongeza kuwa, mkutano huo unaendana na matumaini ya jumuiya ya kimataifa, utasaidia kuhimiza na kutimiza lengo la peninsula ya Korea kutokuwa na silaha za nyuklia, na kusaidia kuleta amani halisi na ya kudumu kwa peninsula hiyo na kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako