• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa walaani shambulizi la kigaidi dhidi ya maeneo ya kuzalisha mafuta Libya

    (GMT+08:00) 2018-06-15 09:05:44

    Tume ya Umoja wa mataifa nchini Libya UNSMIL imelaani shambulizi la kigaidi dhidi ya maeneo yanayozalisha mafuta ya Ras Lanuf na Es Sider nchini Libya, na kusema tukio hilo limeleta hatari kwa uchumi wa Libya, na huenda litazusha mapambano zaidi. Tume hiyo imetoa wito kwa pande zote nchini Libya kujizuia na kulinda umoja wa Libya. Kwa mujibu wa kampuni ya mafuta ya taifa ya Libya, askari watano wa Libya wameuawa, baada ya kundi la kigaidi la Benghazi Defense Brigades, likishirikiana na aliyekuwa kiongozi wa walinzi wa visima Ibrahim Jathran, kufanya shambulizi na kupambana na vikosi vya jeshi la Libya mapema jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako