• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Urari mbaya wa biashara nchini Uganda waongezeka kwa dola bilioni 1.8 katika miezi 9

    (GMT+08:00) 2018-06-15 09:46:29

    Urari mbaya wa biashara kwa Uganda umeongezeka kwa dola za kimarekani bilioni 1.8 katika miezi tisa hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu.

    Akiwasilisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19, Waziri wa fedha, mipango na maendeleo ya uchumi Bw. Matia Kasaija, amesema katika kipindi hicho uagizaji wa bidhaa uliongezeka kwa asilimia 16.4 kwa thamani ya dola bilioni 5.7 za kimarekani, na uuzaji nje wa bidhaa uliongezeka kwa asilimia 9.6 kwa thamani ya dola bilioni 3.93.

    Waziri huyo amesema ongezeko la thamani ya uagizaji wa bidhaa linatokana na kuongezeka kwa bei ya mafuta, na kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa za mtaji zinazounga mkono uwekezaji wa ndani, hasa kwenye sekta ya mafuta na gesi na ujenzi wa miundo mbinu.

    Na ongezeko la uuzaji nje lilitokana na ongezeko la uuzaji wa maharage, Kahawa, chai na mahindi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako