• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kusini na Korea Kaskazini zakubaliana kurejesha mawasiliano ya simu kati ya majeshi yao

    (GMT+08:00) 2018-06-15 10:21:11

    Wizara ya Ulinzi wa Korea Kusini imesema Korea Kusini na Korea Kaskazini zimekubaliana kurejesha mawasiliano ya simu kati ya majeshi yao kwenye sehemu ya mashariki na magharibi, baada ya maofisa waandamizi wa kijeshi wa pande hizo mbili kufanya mazungumzo katika kijiji cha mpakani Panmunjom.

    Majenerali wa pande hizo mbili wamejadiliana kuhusu mambo ya kijeshi kwenye mazungumzo hayo, ambayo ni ya kwanza kufanyika katika miaka 10 iliyopita.

    Kwenye mazungumzo, pande hizo mbili pia zimekubaliana kutekeleza kikamilifu makubaliano yaliyofikiwa mwezi Juni mwaka 2004 kwenye mazungumzo ya majenerali wa majeshi ya pande hizo mbili, yanayolenga kuzuia migongano kwenye eneo la maji la mpaka wa bahari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako