• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi Nigeria waimarisha usalama kabla ya sikukuu ya Eid

    (GMT+08:00) 2018-06-15 10:23:21

    Polisi nchini Nigeria wameimarisha hatua za kiusalama kote nchini kabla ya sikukuu ya Eid el Fitr, ambapo idadi kubwa ya watalii wanatarajiwa kutembelea na kufanya ibada kwenye vituo na bustani.

    Inspekta jenerali wa polisi wa Nigeria Bw. Ibrahim Idris amethibitisha kuwa hatua hizo zinatekelezwa baada ya serikali kutangaza Ijumaa tarehe 15 Juni na Jumatatu tarehe 18 Juni kuwa siku za mapumziko ya kusherehekea sikukuu ya Eid, ikimaanisha kumalizika kwa mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

    Wakati huohuo, polisi nchini humo wamewaua wateka nyara watatu katika operesheni iliyofanyika kwenye jimbo la Taraba, kaskazini mwa nchi hiyo. Kamanda Mkuu wa polisi wa Taraba Bw. David Akinremi amesema watu hao wamewateka nyara watu wengi na kuwashikilia kwenye kambi moja katika kijiji cha Garuwa huko Bali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako