• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la Dunia: Russia yashinda kwa magoli 5 dhidi ya Saudi Arabia

  (GMT+08:00) 2018-06-15 13:13:06

  Michezo ya fainali za kombe la dunia ilianza jana kwa mechi ya ufunguzi kati ya Russia na Saudi Arabia iliyochezwa katika uwanja wa Luzhiniki mjini Moscow. Katika mechi hiyo iliyohudhuriwa na wageni watatu rasimu wakiwa ni Rais Vladmir Putin wa Russia, Mwenyekiti wa FIFA Gianni Infantino na mfalme wa Saudi Arabia. Katika mechi hiyo ambayo ilionyesha kiwango cha chini cha soka na udhaifu wa timu zote, Russia ndio ilikuwa na bahati ya kupata ushindi wa magoli matano kwa bila. Kati ya magoli hayo matano, mawili yalipatikana katika dakika za majeruhi.

  Mechi zinaendelea leo ikiwa timu mbili za Afrika zinatupa karata yao ya kwanza. Misri wanakutana na Uruguay mjini Ekaterinburg, na Morocco wanakutana na Iran mjini St. Petersburg. Mechi ya tatu kwa siku ya leo ni ile ya kundi la kifo, ambapo Ureno ikiwa na nyota wake Ronaldo, inakutana na Hispania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako