• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 9-Juni 15)

  (GMT+08:00) 2018-06-15 19:03:02

  Michuano ya Kombe la Dunia yaanza Urusi

  Michuano ya Kombe la Dunia ya Fifa ya mwaka 2018 imeanza alhamisi nchini Urusi ambapo Urusi wamewatuanga Suadi Arabia mabao 5-0 kwenye mechi ya ufunguzi.

  Mechi ya ufunguzi imehudhuriwa na rais wa Russia Vladmir Putin, mfalme wa Saudia Salman bin Abdulaziz Al Saud na mkuu wa shirikisho la soka duniani Gianni Infantino

  Michuano hiyo itashirikisha mataifa 32, wakiwemo mabingwa watetezi Ujerumani, na itakuwa na mechi 64 zitakazochezwa katika kipindi cha siku 32.

  Fainali itachezwa 15 Julai.

  Fainali za sasa za Kombe la Dunia ambazo ni za 21 zitachezwa katika viwanja 12 katika miji 11 nchini Urusi, ambayo inapatikana eneo la upana wa maili zaidi 1,800.

  Kutokana na hili, kutakuwa na tofauti kubwa katika wakati mechi zinachezwa.

  Ujerumani, waliowashinda Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia 2014, wanapania kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mtawalia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1962.

  Afrika kwenye michuano hii inawakilishwa na Nigeria,Misri, Senegal, Morocco na Tunisia.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako