• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kujibu mara moja hatua ya kibiashara ya Marekani dhidi yake

    (GMT+08:00) 2018-06-15 21:25:02

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng leo amesema, China itajibu hatua za kibiashara zilizochukuliwa na Marekani, ambayo imeamua kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50.

    Bw. Gao amesema, China na Marekani zilifanya duru kadhaa za mazungumzo kuhusu suala la biashara, ili kuondoa mgongano na kutimiza mafanikio ya pamoja, lakini Marekani imepuuza makubaliano yaliyofikiwa, na kuanzisha tena vita vya kibiashara.

    Bw. Gao ameongeza kuwa China itatoa mara moja hatua ya kuongeza ushuru wa forodha dhidi ya bidhaa za Marekani zenye thamani sawa, na matokeo yaliyopatikana kwenye mazungumzo ya zamani yatafutwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako