• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China afanya ziara nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2018-06-17 16:51:40

    Kutokana na mwaliko wa serikali ya Uganda, mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Wang Yang alifanya ziara nchini Uganda kuanzia tarehe 13 hadi 16 mwezi juni, ambapo kwa nyakati tofauti alikutana na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, spika wa bunge la Uganda Bi. Rebecca Alitwala Kadaga na makamu wa Rais Bw. Edward Ssekandi, vilevile amefanya mazungumzo na waziri mkuu wa Uganda Ruhakana Rugunda.

    Wakati alipokutana na Rais Museveni, Bw. Wang Yang amesema China na Uganda zinapaswa kufanya ushirikiano wa pande zote chini ya mfumo wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika na mfumo wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Pia amesisitiza kuwa China inaziunga mkono nchi za Afrika ikiwemo Uganda kutafuta njia za kujiendeleza zinazofuata hali halisi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako