• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sera za kiuchumi za kitaifa zaweza kuathiri biashara ya Nishati ya Marekani

    (GMT+08:00) 2018-06-17 16:56:28

    Sera za kiuchumi za kitaifa zinaweza kuathiri nafasi ya Marekani ya kuwa muuzaji na msambazaji mkuu wa nishatri duniani.

    Marekani inapaswa kuzingatia kwa makini madhara ya kujiondoa katika sera za kibiashara za pande mbalimbali au kukiuka sera za ushirikiano wa nchi mbili baina yake na nchi nyingine.

    Taarifa hii ni kwa mujibu wa matokeo ya utafiki wa kiuchumi kuhusu hali ya biashara ya nishati katika miaka 20 ijayo uliofanywa na Chuo Kikuu cha Houston, nchini Marekani.

    Taarifa hiyo imetolewa siku ambayo serikali ya Marekani imetangaza nyongeza ya asilimia 25 kwenye ushuru wa forodha kwa bidhaa kutoka nchini China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50, ikiwa ni hatua ya nchi hiyo kujitenga na kuanzisha vita vya kibiashara na kuathiri mfumo wa kibiashara wa kimataifa.

    Lakini siku ya ijumaa Wizara ya Biashara ya China, ilisema China kamwe haitaki kushiriki vita vya kibiashara lakini itapigana ili kulinda maslahi ya taifa na wananchi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako