• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwana wa Mfalme wa Cambodia ajeruhiwa katika ajali ya gari, mkewe afariki

    (GMT+08:00) 2018-06-17 18:05:23

    Mwana wa mfalme wa Cambodia Norodom Ranariddh, ambaye pia kiongozi wa Chama cha Funcinpec, amejeruhiwa, na mke wake aitwaye Ouk Phalla amefariki kutokana na ajali iliyotokea mapema jumapili hii baada ya gari lao kugongana na gari jingine aina ya taxi kwenye jimbo la kusini magharibi mwa nchi hiyo la Preah Sihanouk.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kiongozi wa polisi kutoka Preah Sihanouk, mke wa Norodom alifariki majira ya saa sita na nusu mchana kwa saa za Cambodia kufuatia hali ya majeruhi yake kuwa mbaya.

    Ameongeza kuwa, kutokana na majeruhi aliyopata Norodom, ililazimu kumsafirisha kwa haraka kwa njia ya ndege kwenda kupata matibabu katika hospital ya mji mkuu wa nchi hiyo wa Phnom Penh.

    Aidha kamanda huyo wa Polisi amesema, nao abiria watu watano waliokuwa kwenye taxi wamejeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako