• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 34 wauawa kwenye mlipuko wa kujitoa mhanga, na shambulizi la guruneti Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-06-18 09:05:10

    Watu 34 wameuawa na wengine 18 wamejeruhiwa baada ya milipuko pacha na shambulizi la guruneti kutokea jana katika mji wa Damboa, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

    Milipuko hiyo ilifuatiwa na shambulizi la guruneti dhidi ya watu waliokusanyika kuwasaidia majeruhi kwenye eneo la mlipuko wa kwanza. Ofisa wa eneo hilo amesema mlipuko ulitokea usiku wa manane wa jumamosi wakati watu walipokuwa wanarudi kutoka kuangalia matangazo ya mechi ya soka ya kombe la dunia kati ya Nigeria na Croatia iliyochezwa nchini Russia. Haijajulikana kama waliouawa ni wapenzi wa soka.

    Mamlaka za Nigeria hazijasema lolote kuhusu tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako