• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bomu la kutegwa ardhini laua wanausalama 8 wa Kenya mjini Wajir

    (GMT+08:00) 2018-06-18 09:05:28

    Maofisa 8 wa usalama wa Kenya wameuawa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kukanyaga bomu la kutengenezwa kienyeji katika kaunti ya Wajir.

    Mratibu wa eneo la kaskazini mashariki Bw. Muhammed Saleh amethibitisha kuwa tukio hilo limetokea Bojigaras na kulishutumu kundi la Al Shabaab kuwajibika na shambulizi hilo. Amesema waliofariki ni pamoja na polisi watano na wengine watatu wa akiba.

    Tukio hilo limetokea wakati tarehe sita June polisi wa Kenya walitahadharisha kuwa wapiganaji wa kundi la Al Shabaab wanapanga kufanya mashambulizi dhidi ya miundombinu muhimu kwenye eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya ikiwemo mikoa ya pwani wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako