Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limepongeza hatua zilizochukuliwa na Hispania kutatua msukosuko wa uokoaji katika bahari ya Mediterranean baada ya meli ya "Aquarius" iliyokuwa na wahamiaji zaidi 600 waliookolewa, kutoruhusiwa kutia nanga na kushusha wahamiaji nchini Italia na Malta.
Kamishna mkuu wa UNHCR Bw. Filippo Grandi amefurahi kuona msukosuko huo umetatuliwa, lakini amesema tukio hilo halikutakiwa kutokea.
Wahamiaji zaidi 600 waliookolewa wamehamishwa kutoka kwenye meli ya "Aquarius" na kwenda kwenye meli nyingine mbili za Italia, na kuwasili jana katika bandari ya Valencia, mashariki mwa Hispania.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |