• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha utafiti cha China na Afrika chatajwa kuwa muhimu kwa ushirikiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-06-18 09:35:42

    Waziri wa elimu wa Kenya Bibi Amina Mohamed amesema kituo cha utafiti wa pamoja cha China na Afrika kina umuhimu mkubwa kwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye uhifadhi wa mazingira ya asili na utafiti wa teknolojia ya kisasa ya kilimo.

    Bibi Mohamed amesema kupitia jukwaa la kituo hicho, ushirikiano na maingiliano ya kitaaluma kati ya China na Afrika pia umeimarisha zaidi uhusiano kati ya Kenya na China, na Kenya inafurahia ushiriki wa chuo kikuu cha teknolojia ya kilimo cha Jomo Kenyatta kwenye kituo hicho.

    Kituo cha utafiti wa pamoja cha China na Afrika kilichoko ndani ya kampasi ya chuo kikuu cha teknolojia ya kilimo cha Jomo Kenyatta, ni miundo mbinu ya kwanza ya utafiti na mafunzo kujengwa kwa pamoja na China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako