• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taliban yaanza tena mashambulizi dhidi ya jeshi la Afghanistan baada ya kumalizika kwa makubaliano ya kusimamisha vita

    (GMT+08:00) 2018-06-18 17:13:19

    Wapiganaji wa kundi la Taliban wameanza tena mashambulizi dhidi ya jeshi la Afghanistan baada ya makubaliano ya kusimamisha vita kwa siku tatu kumalizika jana usiku.

    Msemaji wa mkoa wa Faryab ulioko kaskazini mwa Afghanistan Abdul Karim Yurash amesema, wapiganaji wa kundi hilo walishambulia vituo kadhaa vya ukaguzi katika wilaya mkoani humo mapema leo, na mapambano bado yanaendelea.

    Serikali ya Afghanistan ilitangaza kusimamisha mapigano kuanzia tarehe 12 hadi 19 ili kulishawishi kundi la Taliban kuunga mkono mchakato mwafaka wa kitaifa. Kwa kujibu wa hatua hiyo, kundi hilo lilitangaza kusimamisha vita kwa siku tatu kuanzia Ijumaa iliyopita, na kumalizika jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako